
MCHEZO mzima wa namna wahamiaji haramu 16 raia wa Somalia na Ethiopia waliokamatwa Jumamosi iliyopita mjini hapa umegundulika.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinasema kwamba, lori hilo lenye namba za usajili T 707 CGY lilikuwa likitokea Ulolo, Tanga likielekea nchi za Zambia na Afika Kusini.…

MCHEZO mzima wa namna wahamiaji haramu 16 raia wa Somalia na Ethiopia waliokamatwa Jumamosi iliyopita mjini hapa umegundulika.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinasema kwamba, lori hilo lenye namba za usajili T 707 CGY lilikuwa likitokea Ulolo, Tanga likielekea nchi za Zambia na Afika Kusini.

“Sisi tulikuwa na mishe zetu pale Msamvu, mara nikashangaa mtu anadondoka akiwa hoi, amechafuka na kitu kama unga, kumbe ni chokaa. Lile gari lilikuwa linajaza mafuta pale. Nikamwambia mwenzangu ndipo tukaamua kutoa taarifa kwa maofisa wa uhamiaji.
“Dereva alionekana kushtukia mchezo, alipomaliza kujaza mafuta, akaliondoa gari kwa kasi. Watu wa bodaboda wakaanza kulifukuza hadi walipokamatwa kule Mzuwanda,” alisema Chambo.
Mmoja wa maofisa wa uhamiaji mkoa wa Morogoro, Wilfred Minja, alithibitisha kukamatwa kwa watu hao ambapo pia aliwashukuru raia wema kwa ushirikiano walioutoa wenye lengo la kulinda usalama wa nchi yetu.

Post a Comment