Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha
Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha
maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa
kumfungua mlangao nyakati za usiku na hivyo kumfanya aamini kuwa
alikuwa na mwanaume mwingine ndani.
Akisimulia mkasa huo huku akiwa wodi
namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume
wake aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa
mbili usiku akiwa amelewa.
"Aliniuliza kwa nini nimechelewa
kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia.Akaaza kunifokea kwamba
nilikuwa na mwanaume mwingine ndani , baadaye akaniomba kurunzi na
panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo kwa kidole" alisema
Ghati.
Wakati anamwonesa lilipo panga na
kumpa kurunzi Ghati hakujuwa nini kinafuata , alifikiri kuwa ni
mambo ya wanaume tu, pengine anataka kwenda sehemu kwa kuwa ndizo tabia
za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia mji kama
uko sawa alafu arudi kulala.
" Alipoipata ile panga akaniambia leo
atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa panga ile akanijeruhi sikio,
mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa kulia ukakatika
kama unavyoona" alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa
amejifunika akiwa amelala kitandani hospitali ya Wilaya Tarime.
Wakati anafanyiwa ukatili huo alipiga
kelele lakini majirani hawakuwahi kufika kumsaidia kwa kuwa ni kawaida
ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika maeneo
hayo.
"Baadaye walikuja na aliposikia
majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia
baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na
kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa"
alieleza .
Jeshi la polisi baada ya kupata
taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha
mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za
kumtia nguvuni kuanza.
Hata hivyo siku moja baadaye Chacha
Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu za wananchi
ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka
hayo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus
Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa , Mwiata alikiri kumsababishia
mke wake ukilema wa maisha.
" Vitendo vya kikatili vilishapitwa
na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha nii jambo lisilo la utu
na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu japo si wote" alisema
Kamugisha kwa nija ya simu
Specially Blog

Home
»
» Unlabelled
» MWANAMKE ALIYE KATWA MGUU NA MME WAKE KISA KACHELEWA KUMFUNGULIA MLAANGO, NI HUKO TARIME.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment