0
Mbunge wa Temeke Mkoani Dar es Salaam, Abbas Mtemvu amezitembelea na kuzifariji familia nne zilizoathirika na janga la moto ulioteketeza makazi yao mwanzoni mwa wiki eneo la Kichangani kata ya Azimio, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akiambatana na Diwani wa Kata ya Azimio Khamis Mzuzuri pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa na kata hiyo Bwana Mtemvu ameshuhudia athari ya moto huo, ambao uliteketeza samani na vifaa vyote na hivi sasa waathirika hao wanaishi kwa majirani.

Katika ziara hiyo fupi, Bwana Mtemvu aliwakabidhi waathirika hao msaada wa vyakula na pesa taslimu ili ziwasaidie katika kipindi hiki kigumu, huku akifanya taratibu kuiomba halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuangalia uwezekano wa kutoa msaada zaidi utakaowawezesha kuendelea kuishi maisha ya kawaida, tofauti na sasa ambapo wanahifadhiwa kwa majirani.

Post a Comment

 
Top