STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby
Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amenusurika kubakwa na vijana wa kihuni
nchini Kenya maarufu kama machokoraa.
Tukio hilo lilitokea pande za Mombasa
nchini Kenya wakati nyota huyo alipokuwa akirekodi video ya wimbo wake
uitwao The Gal Bladder ambapo vijana hao walikatisha shughuli nzima na
kuanza kumkimbiza Baby Madaha.
“Daah! Ilikuwa noma, ilikuwa usiku sasa
wakati meneja wangu akinielekeza matakwa ya video hiyo ambayo yalihitaji
vijana wa mtaani, ghafla wakatokea vijana wenyewe wa mtaani na kutaka
kunibaka. Bahati nzuri nilifanikiwa kutimua mbio na kuwazidi,” alisema
Baby.
Post a Comment